Afariki baada ya kudaiwa kulishwa saruji na askari wa JWTZ

0
40

Mkazi wa Kijiji cha Gumba, Kata ya Gwata wilayani Kibaha mkoani Pwani, Bakari Mbagara (63) amefariki dunia kwa kile kinachodaiwa kuwa alipigwa na waya wa umeme na kulazimishwa kula saruji na Askari wa JWTZ, Koplo Cibumba Lugola wa Kikosi cha 21 FIR Ngerengere.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa amekiri kutokea kwa tukio hilo na kusema wanaendelea kumshikilia mtuhumiwa wa mauaji hayo.

Uchunguzi wa polisi umeonesha kwamba Mbagara ambaye alifariki dunia Januari 2 na kuzikwa Januari 3 alifuatwa kwenye kilabu cha pombe na askari huyo akamchukua kwenda nae eneo analofanyia biashara, akimtuhumu kumuibia kuku wake.

Sahau Bakari ambaye ni mtoto wa marehemu amesema mtuhumiwa baada ya kumpiga baba yake, alimwachia na kumwamuru aondoke, na wakati akirudi nyumbani alianguka njiani.

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend