Afariki kwa kuchapwa viboko 280 baada kumtukana mama yake

0
39

Nelson Mollel (32) mkazi wa Sanawari wailayani Arumeru mkoani Arusha amefariki baada ya kuchapwa viboko 280 na vijana wa mila wa eneo hilo wakishirikiana na baba yake mdogo.

Tukio hilo limefanyika Januari 3 mwaka huu akidaiwa kuwatolea lugha za matusi ya nguoni mama yake mzazi na baadhi ya ndugu siku ya mkesha wa mwaka mpya wakati alipokuwa amelewa.

Mama mzazi wa marehemu, Janeth Kimario amesema baada ya kijana wake kumtuka alimwambia baba yake mdogo, Abel Mboya (45) ambaye alifanikiwa kumpata Nelson na kumpeleka porini na kuanza kumchapa fimbo akiwa na watu wengine.

Akizungumza dada wa marehemu, Jackline Elias Mollel amesema mdogo wake amepigwa viboko 280 badala ya fimbo 70 vinavyopaswa kwa mujibu wa taratibu za mila ya Kimasai.

Raia wa Kenya adukua mifumo ya Zimbabwe na kuiba bilioni 280

“Walimleta wakiwa wamembeba huku na huku hatukujua kilichompata ni nini maana taarifa hatukupewa kwamba anachapwa na mahali alipochapiwa hatukupafahamu yaani tumeletewa mtu na kutupiwa hapo mlangoni, baba yetu mdogo akatamka kwamba tumemleta tumeshampiga itakuwa funzo kwa vijana wengine hawatotukana tena,” mmoja wa ndugu wa marehemu.

Aidha, familia ya marehemu imeiomba Serikali kuchukua hatua za kisheria ili kukomesha tabia hiyo

Send this to a friend