Afariki kwa kunywa pombe akiwa kwenye dozi

0
44

Kijana mmoja anayefahamika kwa jina la Noel Mfoi (20) mkazi wa Sanya Juu Wilaya ya Siha Mkoa wa Kilimanjaro amefarikia dunia kwa madai ya kunywa pombe huku akiwa kwenye dozi, Juni 16 mwaka huu.

Kwa mujibu wa Mtendaji wa Kata ya Sanya Juu, Jonh Dimbo amesema walipofika nyumbani kwa wazazi wa marehemu, walidai mtoto wao alikuwa mgonjwa na alikuwa kwenye dozi, lakini alikunywa pombe ambayo ilisabisha kifo chake.

Katika tukio lingine wilayani humo, mwanaume mmoja amekutwa barabarani katika Kijiji cha Wandri akiwa amefariki kwa kukatwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake.

Diwani wa Kata ya Kirua,  Samweli Mmari amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Juni 17, 2022 ambapo mtu huyo alifahamika kwa jina la utani la  Kiuluulu anayekadiriwa kuwa na zaidi ya miaka 52.

Wazazi washauriwa kuacha kuwalaza watoto na wageni

Aidha, Mmari amesema alipigiwa simu na wasamaria wema wakidai kwamba kuna mtu wamemkuta pembezoni mwa barabara akiwa amejeruhiwa kisha alifika na kupiga simu Kituo cha Polisi Sanya Juu.

“Ni kweli tumeupeleka mwili chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Kibong’oto, ila waliofanya unyama huu hawajafahamika na chanzo cha mauaji hayo bado hakijafahamika, lakini marehemu inadaiwa kuwa ni mwizi katika maeneo mbalimbali ya vijiji vya kata hiyo kwa mujibu wa wakazi wa maeneo hayo.” amesema Mmari

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema wanafuatilia matukio yote hayo.

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend