Uchumi wa Tanzania unatarajia kukua zaidi mwaka 2024 kupita uchumi wa Kenya na Uganda kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).
Katika ripoti mpya ya Utendaji na Matarajio ya Kiuchumi (MEO), AfDB inatabiri kuwa uchumi wa Tanzania utakua kwa asilimia 6.1, ukiwa mbele ya nchi za Afrika Mashariki (Uganda asilimia 6 na Kenya asilimia 5.4) isipokuwa Rwanda ambayo uchumi wake utakua kwa asilimia 7.2.
Tanzania pia inashika nafasi ya tisa kati ya nchi 11 za Afrika ambazo uchumi wake unatarajiwa kufanya vizuri nyuma ya Niger (asilimia 11.2), Senegal (asilimia 8.2), Libya (asilimia 7.9), Rwanda (asilimia 7.2), Côte d’Ivoire (asilimia 6.8), Ethiopia (asilimia 6.7), Benin (asilimia 6.4) na Djibouti (asilimia 6.2). Nchi zinazokamilisha orodha hiyo ni Togo na Uganda ambazo zinatarajiwa kukua kwa asilimia 6 kila moja.
Kampuni za simu zatozwa faini bilioni 2 kwa kukiuka kanuni za usajili wa laini
Rais wa AfDB, Dkt. Akimwumi Adesina amesema inatarajiwa kuwa ukuaji barani Afrika utapanda hadi asilimia 3.8 mwaka 2024, japokuwa linakabiliwa na vikwazo vya ndani kama upungufu wa uzalishaji wa umeme.