Afikishwa mahakamani kwa kuzaa na binti yake

0
36

Mkazi wa kijiji cha Luhagala, kata ya Litumbandyosi wilaya ya Mbinga mkoa wa Ruvuma, Aleyanda Mdendemi (54) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya kwa tuhuma za kufanya mapenzi na watoto wake wawili na kuzaa na mmoja kati yao.

Akisomewa mashtaka hayo na mwendesha mashtaka wa polisi, Inspekta Seilf Kilungwe mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Ally Mkama amedai kuwa mbali na kufanya mapenzi na mabinti zake, pia anatuhumiwa kumuachisha masomo binti yake wa shule ya sekondari.

Mshtakiwa huyo ambaye ni baba mzazi wa watoto hao wawili anadaiwa kutenda makosa hayo katika nyakati tofauti ambapo katika faili la kwanza anatuhumiwa kufanya mapenzi na binti yake (17) mwanafunzi wa kidato cha tatu, Desemba mwaka jana shambani kwao Kata ya Amani Makolo akidai anamtibu kupitia uume wake, kwani binti huyo alikuwa mgonjwa.

Daraja la Tanzanite na Barabara ya Kibaha kuwekewa tozo

Aidha, mwendesha mashtaka ameendelea kudai kuwa mshtakiwa aliendelea kumlaghai binti huyo na kuendelea kufanya naye kitendo hicho kwa kipindi chote wakiwa shambani mpaka waliporudi kijiji cha Luhagala tayari binti yake alikuwa mjamzito na kisha kujifungua mtoto.

Send this to a friend