Afisa Upelelezi akamatwa akidaiwa kuwaachia huru watuhumiwa

0
50

Afisa Upelelezi Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga anashikiliwa na Polisi kwa kudaiwa kuwaachia huru watuhumiwa wa uhujumu uchumi waliokamatwa na mali za magendo zenye thamani ya zaidi ya TZS bilioni 1.2.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba amesema Septemba 09, 2022 walikamata Jahazi lililobeba baro 170 za vitenge vinavyokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 570 na watu wanne wakihusishwa na usafirishaji huo, huku Septemba 11 Kamati ya Ulinzi ilikamata watu 20 na malori mawili aina ya fuso yakiwa na baro 90 za vitenge kila moja.

“Nimeshangazwa kuona watuhumiwa wote wanne waliokamatwa na Jahazi wameachiwa huru bila ya taarifa na hawajafunguliwa kesi kama vile hakuna walichofanya. Pia watuhumiwa 15 kati ya 20 ambao walikamatwa na baro 180 za vitenge nao wameachiwa huru ingawa wamefunguliwa kesi za uhujumu uchumi,” amesema.

Mtoto asafiri zaidi ya 460km kwenye uvungu wa basi

Mgumba amesema alipofanya kikao na kamati hiyo ndipo akabaini Afisa Upelelezi Wilaya ya Mkinga ndiye aliyehusika na kuachiliwa kwa watuhumiwa hao huku akidai amepewa maelekezo na Afisa Upelelezi Mkoa ambaye hakuwepo katika kikao hicho.

Aidha, mkuu huyo wa mkoa amesema afisa huyo wa upelelezi tayari yupo ndani na sheria itafuata mkondo wake.

Send this to a friend