Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika ambaye pia ni Rais wa Senegal, Macky Sall anasafiri kuelekea nchini Urusi kujadili mzozo wa chakula uliosababishwa na vita ya Urusi na Ukraine.
Ofisi ya Rais Sall imesema ziara hiyo inalenga kukomboa akiba ya nafaka na mbolea ambayo kwa sasa imezuiwa katika bandari za Ukraine.
Aidha, Rais Sall anatazamiwa kukutana na Rais wa Urusi, Vladimir Putin siku ya Ijumaa nchini humo.
Agizo jipya la Waziri Nape kwa TCRA na kampuni za simu kuhusu bando
Taarifa zinaeleza kuwa mataifa ya Afrika yameathiriwa zaidi na ongezeko la bei lililosababishwa na vita hivyo.