Afrika Kusini: Bondia aliyeonekana akirusha ngumi hewani afariki dunia

0
63

Shirikisho la Ngumi za Kulipwa nchini Afrika Kusini, pamoja na familia ya Buthelezi imethibisha kutokea kwa kifo cha bondia, Simiso Buthelezi aliyefariki usiku wa Juni 7 hospitalini, Durban.

Buthelezi alishiriki pambano la ubingwa lililoandaliwa na Starline Boxing Promotions huko Greyville, Durban dhidi ya Siphesihle Mntungwa wikendi iliyopita na kumwangusha mpinzani wake katika raundi ya 10.

Hata hivyo, katika matukio ya ajabu na ya kutisha, ni Buthelezi ambaye alipoteza pambano muda mfupi baadaye, huku akionekana kurusha ngumi hewani. Baada ya hali hiyo isiyo ya kawaida, mwamuzi aligundua kuwa kuna kitu hakikuwa sawa kwake na akakatisha pambano hilo.

Bondia huyo alikimbizwa hospitalini baada ya kupoteza fahamu na kugundulika kuwa ubongo wake ulipata majeraha yaliyosababisha kuvuja damu kwa ndani, tatizo lililopelekea kifo chake.

Shirikisho hilo limesema linaendelea kufanya uchunguzi wa tukio hilo, na kisha itaweka hadharani matokeo ya ukaguzi huo.

Send this to a friend