Afrika Kusini: Watu 10 wa familia moja wauawa kwa risasi

0
46

Watu kumi wa familia moja, wakiwemo wanawake saba na wanaume watatu wameuawa na watu wenye silaha siku ya Ijumaa katika mji wa Pietermaritzburg, jimbo la KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini.

Inaaminika kuwa watu wawili wenye silaha waliingia kwenye nyumba hiyo na kufyatua risasi kwa familia hiyo, na kwa mujibu wa polisi chanzo cha mauaji hayo bado hakijajulikana.

Msemaji wa polisi wa kitaifa Athlenda Mathe ameiambia CNN kuwa baadhi ya watuhumiwa wa tukio hilo tayari wamekamatwa.

Watu 78 wafariki wakipatiwa msaada wa Ramadhan

“Washukiwa wawili wamekamatwa, mmoja amekufa, mwingine alikimbia eneo la tukio. Polisi wanaendelea na msako,” amesema na kuongeza kuwa bunduki tatu zimepatikana kutoka kwa washukiwa hao.

Afrika Kusini imekumbwa na visa vingi vya ufyatuaji risasi katika miezi ya hivi karibuni huku matukio mengine yakihusishwa na magendo ya dawa ya kulevya.