Afrika Kusini yamuunga mkono Dkt. Tulia Urais wa IPU

0
54

Afrika Kusini imemuunga mkono, Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt Tulia Ackson ambaye anagombea kiti cha Urais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).

Spika wa Bunge la Afrika Kusini, Mapisa-Nqakula ameweka wazi hilo wakati akiongoza ujumbe wa wabunge wa Afrika Kusini kwenye kikao cha Kamati Tendaji ya Mabunge ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC PF) (EXCO) uliofanyika mjini Mahe, Shelisheli.

“Tunaamini kuwa IPU inahitaji kijana na mtu mahiri mwenye mawazo mapya ili kupeleka IPU mbele na kuhakikisha kuwa mabadiliko yanafanyika pale inapobidi. Dkt. Ackson ana ujuzi unaohitajika kwa jukumu hilo,” amesema.

Aidha, amesema nchi nyingine za SADC zitaanza kushawishi makundi mengine ndani ya bara hilo kumuunga mkono Ackson ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kundi la Afrika katika Umoja wa Mabunge Duniani.

IPU ni taasisi ya kimataifa la mabunge ya kitaifa ambayo linawezesha mabunge na wabunge kukuza amani, demokrasia na maendeleo endelevu.

Send this to a friend