Afrika Kusini yapinga vitu vya Hayati Mandela kupigwa mnada Marekani

0
14

Serikali ya Afrika Kusini inaendelea na jitihada za kuzuia mnada wa vitu vya shujaa wa kupinga ubaguzi wa rangi, Hayati Nelson Mandela, unaofanywa na binti yake mkubwa Makaziwe Mandela, nchini Marekani.

Mnada huo, unaojumuisha vitu 70 vya Mandela, umepangwa kufanyika Februari 22 ikiwa ni sehemu ya jitihada za kupata fedha ili kusaidia kuanzisha bustani ya kumbukumbu karibu na eneo ambapo rais huyo wa zamani amezikwa.

Miongoni mwa vitu hivyo 70 vinavyotarajiwa kuuzwa ni kitambulisho cha awali cha Mandela cha mwaka 1993, miwani yake ya jua na kusomea, mashati yake maarufu ya Madiba, fimbo zake za kutembelea, mikoba yake, raketiboli yake ya tenisi ya Robben Island, vifaa vyake vya kusikia, na kadhalika.

Mwezi uliopita, waandaaji wa mnada huo, wakiongozwa na binti mkubwa wa Mandela, Dkt. Makaziwe, walishinda uamuzi wa mahakama baada ya maafisa wa Afrika Kusini kujaribu kuzuia uuzaji wa vitu hivyo.

Hata hivyo, serikali inasisitiza kwamba bidhaa hizo ni mali ya taifa na hazipaswi kuchukuliwa nje ya Afrika Kusini kulingana na sheria za nchi hiyo, huku Wakala wa Rasilimali za Urithi wa Afrika Kusini (Sahra), chombo cha serikali kinachosimamia historia na utamaduni wa nchi hiyo, kikifungua rufaa ya kuzuia mnada huo.”

Send this to a friend