Afrika yatokomeza ugonjwa wa Polio

0
60

Afrika imepiga hatua kubwa katika sekta ya afya baada ya kufanikiwa kutokomeza ugonjwa wa polio, Nigeria ikiwa ni nchi ya mwisho kuwa na muathirika wa mwisho wa ugonjwa huo.

Ugonjwa wa Polisi huwaathiria watoto chini ya miaka mitano ambapo miongoni mwa athari zake ni ulemavu wa kudumu na kifo huweza kutokea endapo misuli ya upumuaji inapoathiriwa.

Ugonjwa huo hauna dawa, lakini chanjo yake humlinda mtoto kwa maisha yake yote.

Agosti 25, 2020, Shirika la Afya Duniani (WHO) liliitangaza Nigeria kuwa haina ugonjwa wa Polio na hivyo kuifanya Afrika kutokuwa na mgonjwa yeyote. Hii ni mara ya pili kwa Afrika kutokomeza virusi ambapo miaka 40 iliyopita virusi vya small pox vilitokomezwa.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Adhanom Ghebreyesus amesema “hili ni moja ya mafanikio makubwa sana ya kiafya.”

Baada ya Afrika kutokomeza ugonjwa huo, sasa umebaki katika nchi za Afghanistan na Pakistan.

Hata hivyo, njia zilizotumika kukabiliana na maambukizi ya virusi hivyo barani Afrika zimeshindwa kuzaa matunda katika vita dhidi ya virusi vya corona. Njia hizo ni pamoja na kufuatilia waathirika kwa njia ya simu (smartphone-enabled tracing), ushirikishwaji wa serikali za mitaa, ushirikiano wa kimaabara kwa nchi 15 na ufuatiliaji wa vinasaba (genetic sequencing) kuweza kufahamu chanzo cha mlipuko.

Send this to a friend