AFRIMMA yamtunuku Rais Samia Tuzo ya Uongozi Bora

0
36

Rais Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Tuzo ya Uongozi kwa mwaka 2022 inayotolewa na AFRIMMA kwa kutambua mchango wake katika kukuza tasnia ya sanaa na burudani nchini Tanzania.

AFRIMMA imesema kuwa Rais Samia ameweka mfano ambao utaigwa na viongozi wengine kwa kuboresha taswira ya burudani nchini Tanzania.

“Kutoka kufufua Tuzo za Muziki Tanzania hadi kuboresha usimamizi wa mfumo wa hatimiliki ambao hukuza uwezo wa kiuchumi wa wasanii, Rais Samia ameacha alama isiyofutika katika historia ya Tanzania,” taarifa ya AFRIMMA imeeleza.

Aidha, imempongeza kwa kutumia siku nane nje ya ofisi kuandaa filamu ya Tanzania: The Royal Tour ambayo alikuwa mwongoza watalii akiionesha dunia uzuri wa Tanzania.

Kutokana na hayo na kuweka sera bora, kuonesha mapenzi yake kwenye sanaa AFRIMMA imesema ni faraja kwao kumtunuku Tuzo ya Uongozi mwaka 2022.

Send this to a friend