Afungwa jela miaka 10 kwa kuwabaka mbwa 42

0
79

Mtaalamu mashuhuri wa mamba nchini Australia, Adam Britton amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela baada ya kukiri kuwabaka na kuwatesa mbwa zaidi ya 42 na baadhi kuwasababishia kifo.

Mtaalamu huyo wa elimu ya wanyama mwenye umri wa miaka 53 ambaye amewahi kufanya kazi kwenye shirika la BBC National Geographic, amekiri mashtaka 56 yanayohusiana na unyama na ukatili wa wanyama.

Mahakama ya Juu ya Eneo la Kaskazini (NT) imesema mwanaume huyo alikuwa akijirekodi akiwatesa wanyama hao na wengi wao kufariki, kisha alizichapisha video hizo mtandaoni kwa kutumia majina bandia.

Britton alikamatwa Aprili 2022 baada ya upekuzi katika eneo lake kijijini Darwin, ambapo katika hukumu yake pia amepigwa marufuku kununua wanyama na kuwafuga kwa kipindi chote cha maisha yake.

Send this to a friend