Afungwa maisha kwa kumbaka mwanafunzi wa darasa la kwanza

0
100

Mahakama ya Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa imemhukumu kifungo cha maisha jela Justine Ludege (20) mkulima na mkazi wa kijiji cha Utengule wilayani humo kwa kosa la kubaka mwanafunzi wa darasa la kwanza mwenye umri wa miaka sita.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Jeshi la Polisi imesema mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo Januari 02, mwaka huu katika Kijiji cha Utengule wilayani Kilolo, ambapo alikutana na mhanga barabarani na kumvutia porini kisha kumfanyia kitendo hicho.

Aidha, imeeleza kuwa kutokana na mhanga kumtambua mshitakiwa, alitoa taarifa kwa mama yake ambapo Jeshi la Polisi lilimkamata na kumfikisha mahakamani ambapo kufikia Julai 30, 2024 mshitakiwa alikutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.

Send this to a friend