Afya: Jinsi ya kutumia kitunguu saumu kumaliza chunusi usoni

0
121

Ni wazi kuwa hakuna mtu anayependa kuwa na chunusi usoni, ndio maana baadhi huenda mbali na kutumia gharama kubwa kununua vipodozi vitakavyowawezesha kuwa na ngozi nyororo yenye kupendeza.

Katika meza ya afya leo tumekuja na jawabu la tatizo lako kwani hauhitaji kutumia gharama kubwa kupata ngozi nyororo, sasa utahitaji tu kitunguu saumu kufanikisha hilo.

Kitunguu saumu ni moja ya viungo vinavyozuia  bekteria mbalimbali wa ngozi na kuzuia chunusi. Vitunguu saumu vilivyotwangwa vikipakwa katika chunusi zilizotumbuliwa na kuachwa kwa hadi dakika tano inasaidia kutibu vidonda hivyo na kuiacha ngozi ikiwa laini na isiyo na weusi.

Kitunguu hicho kinapunguza ukubwa wa chunusi na kuifanya isinyae. Pia, unaweza kuzuia matatizo ya ngozi kwa kuweka kitunguu saumu kwenye chakula chako.

Unashauri kukichanganya na maji kabla ya kupaka usoni mwako ili kupunguza nguvu yake, tofauti na ukikipaka bila kukichanganya na maji.

Send this to a friend