Afya: Nafasi ya vitamini C katika kukukinga dhidi ya corona

0
43

Wakati dunia ikiendelea na mapambano dhidi ya mlipuko wa virusi vya corona, watu wameendela kuchukua tahadhari mbalimbali kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi hivyo, huku wengine ambao tayari wameathirika wakiendelea na matibabu.

Hata hivyo, baadhi ya tahadhari zinazochukuliwa kujikinga na COVID-19 zimezua mjadala kama kweli zinaweza kumkinga mtu asipate virusi hivyo vinavyosababisha homa ya mapafu. Moja ya njia zilizoibua mjadala ni nafasi ya Vitamini C katika kumkinga mtu dhidi ya corona.

Vitamini C ni virutubisho vinavyopatikana katika matunda na mboga mbalimbali, lakini pia kuna vidonge vya virutushio hivyo, ambapo kutokana na kasi ya kusambaa kwa COVID-19, kumekuwa na ongezeko la watu kutumia virutubisho hivyo wakiamini kwamba wanajiweka salama.

Ni sahihi kuwa Vitamini C inaimarisha kinga ya mwili, lakini hakuna ushahidi wa kitabibu kuwa utumiaji wake utaweza kukukinga usipate COVID-19.

Vitamini C husaidia kumpunguza kwa kiasi kikubwa haki ya ubaridi wa mwili inayosababishwa na virusi, lakini hii haimaanishi moja kwa moja kuwa virutubisho hivyo vitakuwa na athari sawa kwenye virusi vya corona.

Pia, vitamini C huyeyuka kwenye maji ndani ya mwili, hii ina maana kuwa vitamini za ziada hutolewa nje ya mwili kwa njia ya mkojo. Hivyo ulaji wa kiasi kikubwa cha virutubisho hivyo hakumaanishi kwamba mwili wako utaongeza kiasi cha matumizi.

Ulaji wa kiwango kikubwa cha vidonge vya vitamini C kunaweza kukapelea mtu kuharisha, kutokana na kuupa mwili taarifa ya kutoa maji ndani ya seli na mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.

Hata hivyo, unashauriwa kutumia virutubisho hivyo kwa kiwango kinachotakiwa kwani ni muhimu katika kuimarisha kinga ya mwili.

Kutokana na COVID-19 kutokuwa na dawa, unashauriwa kuepuka mikusanyiko ya watu, kuhakikisha unakuwa katika hali ya usafi muda wote, kuvaa barako, kufunika mdomo/pua unapokohoa au kupika chafya.

Send this to a friend