Agizo la polisi kwa mabasi ya abiria kuelekea Desemba
Jeshi la Polisi limetoa onyo kwa wamiliki na waendeshaji wa vyombo vya moto, hasa mabasi ya abiria watakaokiuka sheria za usalama barabarani kwa kuzidisha abiria kwa lengo la kujipatia fedha zaidi.
Polisi wamesema watu hao wanaotaka kujipatia fedha bila kujali usalama na maisha ya wengine waache tabia hiyo mara moja, kwani hatu kali zitachukuliwa dhidi yao.
Taarifa ya polisi imeeleza kwamba kumekuwa na tabia inapoelekea mwisho wa mwaka na mwanzo wa mwaka, kutokana na wingi wa abiria, mabasi ya abiria yamekuwa yakiweka vigoda, stuli au ndoo kwenye njia za kupita abiria ili abiria wengi zaidi wakae.
Tayari baadhi ya madereva na makondakta wamekamatwa kwa vitendo hivyo, na wananchi wameshauriwa kuendelea kuvifichua ili kuvikomesha.