Agizo la Polisi kwa wapenzi wanaotumiana picha za utupu

0
73

Jeshi la Polisi limewataka wasichana na wanawake kujitahadharisha na wapenzi au marafiki zao wanaowadanganya wajipige picha za utupu kisha wawatumie.

Taarifa ya jeshi hilo imeeleza kwamba baadhi ya wanawake waliowatumia wapenzi au marafiki zao picha hizo walianza kuwataka wasichana wawape fedha la sivyo watazisambaza kwenye mitandao ya kijamii.

“Baadhi ya wakina dada wamejikuta katika matatizo ikiwa ni pamoja na msongo wa mawazo, kushindwa kufanya shughuli zao za kujiletea maendeleo na wengine kushindwa kufuata masomo darasani na kupelekea kushuka kiwango,” imeeleza taarifa hiyo.

Jeshi hilo limewatahadharisha wananchi juu ya utapeli mwingine wa wahalifu kutumia majina ya viongozi wa serikali na viongozi wastaafu kuwa wamefungua asasi za kiraia (NGOs) au mashirika ya kukopesha fedha, hivyo kuwataka watu watume fedha kwa ajili ya usajili ili wapate mikopo.

Send this to a friend