Agizo la serikali kuhusu miradi ya Morocco Square na Mji wa Kawe

0
32

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt Angeline Mabula amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Mkandarasi Kampuni ya Ujenzi ya Estim Construction kuhakikisha mradi wa ujenzi wa Morocco Square unakamilika kufikia Juni 30, 2022.

Kauli hiyo ya Dkt Mabula inafuatia uamuzi wa serikali kuiruhusu NHC kukopa fedha kwa ajili ya kumaliza mradi huo uliokuwa umesimama kwa takriban miaka mitatu sasa.

Kwa mujibu wa Msimamizi wa mradi huo kutoka shirika holi, Samuel Metili, mradi wa Morocco Square unaogharimu shilingi bilioni 137.5 ulisimama tangu mwaka 2017 kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ile ya kifedha na mabadiliko ya baadhi ya maboresho kwenye maeneo ya majengo hayo.

Alisema, kwa sasa ujenzi huo unaojumuisha nyumba za makazi kwa ajili ya kuuza na kupangisha, maduka makubwa ya biashara (Mall), ofisi, kumbi za cinema, mabenki pamoja na hteli unaendelea na umefikia asilimia 90.

Akizungumzia mradi wa Mji wa Kawe, Dkt Mabula alilitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuharakisha mazungumzo ya uwekezaji na Mwekezaji Mwenza Kampuni ya Al-Gurey-Dubai kuhusiana na mradi huo na kusisitiza kuwa, ni vizuri NHC ikawa mipango thabiti ya uendelezaji mji huo.

Moja ya jengo katika mradi wa ujenzi wa Mji wa Kawe mkoani Dar es Salaam ambao ujenzi wake ulisimama kwa muda mrefu.

“Kuhusu mradi wa Kawe ni vizuri kujua future plan ya eneo na ni vizuri kila eneo la Shirika la Nyumba likafanyiwa maandalizi ya kitu kinachotaka kufanyika. Yale maeneo ambayo ni ‘prime’ muyaainishe na kuyaendeleza maana hata NHC inaweza kunyang’anywa.” alisema Dkt Mabula.

Send this to a friend