Agizo la Serikali kwa shule zinazochuja wanafunzi wasiofikisha viwango vya ufaulu

0
45

Serikali imepiga marufuku baadhi ya shule kuchuja wanafunzi wasiofikia kiwango kilichowekwa na shule pamoja na kuwazuia kufanya mitihani ya kitaifa kwa wanafunzi ambao hawajalipa ada.

Akizungumza Ofisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Abdul Maulid amesema Serikali haikubaliani na hali hiyo ambayo huwasababishia wazazi msongo wa mawazo pindi wanapopewa taarifa za watoto kuchujwa wanaposhindwa kufikia kiwango.

Waziri Nchemba: Serikali imeunda timu ya wataalam kuchambua tozo zenye utata

“Unakuta mtoto amesoma kidato cha kwanza hadi cha nne, wakati wa mitihani shule inaweka vigezo vyake kwamba huyu aondoke, aondoke aende wapi wakati muda wote amesoma shuleni kwako, hiyo hatutakubali tunataka amalizie hapo hapo kwako aliakoanzia na hatutaki arudie darasa,” ameonya.

Ameongeza kuwa “mtoto amekuja kwako akiwa vizuri umekaa naye, na kama kuharibika kaharibikia shuleni kwako, sasa unataka kumpeleka kwa nani? Hili halikubaliki hata kidogo, tupeni taarifa ya shule hizo zenye tabia ya kuondoa watoto kwenye siku za mitihani.”

Aidha, amebainisha kuwa hakuna sheria inayoruhusu mtoto kurudia darasa kwa sababu hajalipa ada, hivyo amezitaka shule za Dar es Salaam zikutane na wazazi na kutatua changamoto za ada kabla ya mitihani.

Send this to a friend