AGRICOM YAKABIDHI TREKTA 500, POWER TILLERS 800 NA VIFAA VINGINE VYA KILIMO.

0
41

 

kampuni ya Kitanzania ya Agricom imekabidhi vifaa na zana mbalimbali za kisasa za kilimo kwa serikali kupitia Wizara ya Kilimo, wakati wa maonyesho ya Nane Nane yaliyofanyika Dodoma leo.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Rais wa Tanzania, Mheshimiwa Dokta Samia Suluhu Hassan, ambaye alishuhudia makabidhiano hayo.

Vifaa na zana zilizokabidhiwa kwa serikali ni pamoja na Trekta 500, Power tillers 800 pamoja na Vifaa vya maandalizi ya shamba 200.

Makabidhiano haya ni sehemu ya mpango wa serikali wa “Agenda 10/30: Kilimo ni Biashara,” unaolenga kuboresha kilimo nchini kwa kuwapatia wakulima zana bora zinazoongeza ufanisi na uzalishaji. Hii inatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika kuendeleza sekta ya kilimo, kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa na kuimarisha usalama wa chakula nchini.

Send this to a friend