Ahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kumbaka mtoto wake wa kambo wa miaka mitatu

0
65

Mahakama ya Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha imemhukumu kifungo cha maisha jela, John Sanare Lukuaya (23) mkazi wa Kijiji cha Kimnyaki, Kata ya Kimnyaki kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka mitatu na miezi miwili ambaye anasadikika kuwa ni mtoto wa mke wake.

Akitoa hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Wilaya, Gwantwa Mwankunga amesema mahakama imefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa pasipo shaka yoyote na kumtia hatiani mtuhumiwa huyo.

Mwendesha Mashitaka na Wakili wa Serikali, Penina Ngotea ameieleza mahakama kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Julai 10 ,2022 katika Kijiji cha Kimnyaki ndani ya nyumba wanayoishi na mtoto huyo.

Mwenyekiti wa UVCCM auawa baada ya kufumaniwa

Amefafanua kuwa mtuhumiwa alifanya tukio hilo usiku wakati mama wa mtoto huyo akiwa amekwenda kulala kwenye msiba wa jirani na kuamwacha mtuhumiwa akiwa amebaki na mtoto usiku huo.

Afisa Ustawi wa Jamii halmashauri ya Arusha, Beatrice Tengi ameipongeza mahakama kwa kutenda haki na kuhakikisha haki ya mtoto huyo inapatikana.

Send this to a friend