Ahukumiwa kifungo cha maisha mara mbili kwa kumlawiti mwanafunzi

0
64

Emanuel Gwandu (21) amehukumiwa kifungo cha maisha mara mbili jela pamoja na kulipa fidia ya TZS milioni 5 baada ya kukutwa na hatia ya kulawiti mwanafunzi mwenye umri wa miaka 13.

Gwandu mkazi wa Mtwivila maarufu kama Master Play Station aliyekuwa akisimamia sehemu ya kuchezesha michezo ya video, alidaiwa kumrubuni mwanafunzi huyo kwa kumpa nafasi kucheza bila malipo na kisha kumpeleka vichakani na kumuingilia kinyume na maumbile.

Mahakama hiyo imemshtaki mtuhumiwa kwa makosa mawili aliyotenda kwa terehe tofauti mwezi Agosti na kosa la pili Septemba 27 ambapo alimuingilia mwanafunzi huyo mara 6 kinyume na maumbile.

Akisoma hukumu hiyo, Hakim Mkazi Mkuu Said Mkasiwa amesema kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamni hapo, mtuhumiwa alitumia fursa ya mwanafunzi huyo ya kukosa pesa na mapenzi yake ya kucheza play station kumfanyia ukatili huo.

Aidha, mtuhumiwa alipopewa nafasi ya kujitetea aliiomba mahakama hiyo kumpunguzia adhabu kwakuwa hajatenda kosa lolote.

Send this to a friend