Ahukumiwa kuchapwa viboko 12 kwa kumlawiti mwanafunzi

0
62

Mwanafunzi ya Kidato cha Tatu, Hija Hamis Msumi (16) mkazi wa Kijiji cha Nyanjati wilaya ya Kibiti amehukumiwa adhabu ya kuchapwa viboko 12 kwenye makalio mbele ya mahakama kwa kosa la kumbaka na kumlawiti mwanafunzi wa darasa la Nne mwenye umri wa miaka 12.

Mahakama imeeleza kuwa mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo kati ya mwezi Agosti na Novemba, 2023 huko Kijiji cha Nyanjati wilaya ya Kibiti.

Taarifa ya mahakama imeeleza kuwa, Septemba 26, 2024 baada ya shauri hilo kusikilizwa mpaka mwisho kwa upande wa mashitaka kuwaleta mahakamani mashahidi saba pamoja na ushahidi wa nyaraka mbili, shitaka lenye makosa mawili ya kubaka na kulawiti lilithibitishwa na mshitakiwa alikutwa na hatia.

Aidha, Mahakama imemuamuru mshitakiwa huyo kumlipa muhanga fidia ya Shilingi laki 5 kwa madhara ambayo amemsababishia mwanafunzi huyo ambaye jina lake limehifadhiwa.

Send this to a friend