Ahukumiwa miaka 30 kwa kumbaka na kumpa ujauzito mtoto wa shemeji yake

0
41

Mahakama ya Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Michael Mchanjale (31) kwa kosa la kumbaka na kumpa ujauzito mtoto wa dada wa mke wake mwenye umri wa miaka 14.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Septemba 22, 2023 saa tatu usiku wakati mtoto huyo alipokwenda nyumbani kwa mshtakiwa kwa lengo la kujihifadhi mara baada ya kupigwa na kufukuzwa na mama yake wa kambo anayeishi naye.

Kabla ya hukumu hiyo, upande wa Jamhuri uliowakilishwa na wakili wa serikali, Elias Masini uliiomba mahakama itoe adhabu inayostahili ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaokwamisha ndoto za mabinti wengi.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Irene Lyatuu amesema mahakama imempa adhabu hiyo baada ya kuzingatia ushahidi wa pande zote mbili, na kwamba rufaa ya hukumu hiyo iko wazi kwa upande ambao haujaridhika na uamuzi uliotolewa ndani ya muda wa kipindi cha siku 30.

Send this to a friend