Ahukumiwa miaka 30 kwa kumgeuza binti yake mke wake

0
41

Michael John Christopher maarufu kama ‘Omoro’ mkazi wa Nyambiti, Ngudu Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza amehukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kumbaka binti yake wa kambo (14).

Awali, mshtakiwa alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kwimba Aprili 9,2024 na kusomewa shitaka hilo ambapo mshitakiwa alikana kutenda kosa na kesi kuahirishwa hadi Aprili 24, 2024 kwa ajili ya kusomewa hoja za awali.

kwa mujibu wa hati ya mashtaka, mshtakiwa alitenda kosa hilo kwa nyakati tofauti kati ya Desemba 12,2023 hadi Machi 25,2024 katika mtaa wa Majengo Nyambiti ndani ya wilaya ya Kwimba na Mkoa wa Mwanza.

Mahakama imeeleza kuwa mshitakiwa alianza kufanya mapenzi na binti huyo tangu mwaka 2022 wakiwa Wilaya ya Rorya Mkoa wa Mara kabla hawajahamia mkoani Mwanza, baada ya mama mzazi wa binti hyo kufariki dunia na kumuacha mikononi mwa baba huyo wa kambo.

Baada ya kuhamia Mkoa wa Mwanza, mtuhumiwa aliendelea kufanya mapenzi na binti huyo hadi ilipofika Machi 25,2024 ambapo binti alikataa kufanya mapenzi na baba yake wa kambo baada ya kushauriwa kutofanya hivyo na mama yeke mkubwa, hali iliyopelekea baba huyo kumpiga binti yake kwakile alichodai kumnyimba unyumba.

Hata hivyo, mshitakiwa alipopewa nafasi ya kujitetea alisema kwamba alikuwa akilala chumba kimoja na binti huyo baada chumba kingine kukirudisha kwa mwenye nyumba kwa kushindwa kulipa kodi ya chumba cha pili ambapo utetezi huo ulitupiliwa mbali na mahakama.

Send this to a friend