Ahukumiwa miaka 5 jela kwa kujirekodi akila popo

0
39

Mwanamke mmoja raia wa Thailand, Phonchanok Srisunaklua amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela baada ya kurekodi video ambayo inasambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha akila popo.

Mwanamke huyo alirekodi kipande hicho kwenye ukurasa wake wa Facebook, akionesha popo waliokuwa kwenye bakuli la supu na kuanza kuwakunjua mbawa zao kabla ya kuanza kuwala huku akiwaelezea jinsi walivyo na ladha nzuri.

Video hiyo imeleta upinzani mwingi kutoka kwa watumiaji wa mtandao ambao waliibua wasiwasi kuhusu athari za kiafya za vitendo vya Srisunaklua huku mmoja wa madaktari wa mifugo akikemea kitendo hicho kwa kuwa popo wana vimelea vingi vya magonjwa na hakuna uthibitisho kwamba maji ya moto yanaweza kuua vijidudu hivyo.

Mwanaume aiba ng’ombe na kuiuza ili amnunulie mchumba wake zawadi

Aidha, vyombo vya habari vya ndani vimeripoti kwamba mwanamke huyo alichapisha video ya kuomba msamaha kwa jamii, madaktari, waandishi wa habari, wafanyakazi wenzake, familia na marafiki dhidi ya kitendo hicho.

Sasa mwanamke huyo anakabiliwa na kifungo cha miaka mitano jela au faini ya hadi takribani TZS milioni 32.5 kwa kumiliki mizoga ya wanyamapori na kwa uhalifu unaokiuka Sheria ya Makosa ya Kompyuta (2007).

Send this to a friend