Aina 10 za magari yanayotumika zaidi Dar es Salaam

0
138

Kama umekuwa ukizunguka katika sehemu nyingi za jiji la Dar es salaam, bila shaka utakuwa unakumbana na aina fulani ya magari ambayo unakutana nayo kwa wingi.

Haya ni aina ya magari ambayo hutumiwa sana na Watanzania katika jiji la Dar es salaam katika shughuli zao mbalimbali za kila siku.

Toyota IST
Toyota IST ni moja ya magari yanayoongoza kwa kutumiwa na watu wengi hususani katika jiji la Dar es Salaam. Kutokana na urahisi katika umiliki na utumiaji mdogo wa mafuta, IST imekuwa chaguo namba moja kwa wengi ambao hawana matumizi makubwa.

Subaru Impreza
Hili ni moja ya magari yanayotumiwa sana katika jiji la Dar es Salaam, injini yake ina uwezo hadi cc2,212.

Toyota Corolla Rumion
Toyoya Corolla Rumion ni moja kati ya magari yenye mwonekano mzuri na yanayoendeshwa sana katika jiji la Dar es Salaam.

Toyota Ractis
Kutokana na mwonekano kiumbo na gharama nafuu za umiliki na uendeshaji, Ractis imekuwa chaguo la watu wengi ambao hawana matumizi makubwa sana ya gari.

Subaru Forester
Forester ambayo ni gari la pili kutoka kampuni ya Subaru imekuwa kivutio cha watu wengi hususani vijana, jambo linalosababisha kuwepo kwa wingi katika sehemu nyingi za Dar es Salaam.

Toyota Corolla Spacio
Hizi pia ziko nyingi. Toyota Corolla Spacio ni gari nzuri ambazo zinatajwa kutokuwa na gharama katika matumizi, na ndiyo sababu ya kupendwa na watu wengi.

Toyota Premio
Katika miaka ya karibuni, Toyota Premio imekuwa kivutio kikubwa kwa watu wengi wanawake kwa wanaume. Umbo mwonekano na uimara vimekuwa sababu ya magari haya kutumiwa na watu wengi.

Toyota Alphard
Hii ni gari inayofaa sana kwa matumizi ya familia na ofisi kwani ina nafasi kubwa na mwonekano wa kifahari. Gari hii pia hupendwa na watu wengi.

Toyota Harrier
Kama ilivyo kwa Toyota Alphard, gari hii pia inafaa kwa matumizi ya familia na matumizi ya ofisi kutokana na nafasi yake kuwa kubwa. Watu wengi huipenda gari hii kwa kuwa pia ina mwonekano wa kifahari.

Toyota Crown
Crown wamiliki wake hujiita “Royality” yaani wanafamilia na ukoo wa kifalme. Ina injini yenye uwezo wa cc1,988 hadi cc2,997 na imekuwa kivutio kikubwa kwa watu wengi kutokana na muonekano wake.

Send this to a friend