Aina 10 za watumiaji wa mitandao ya kijamii

0
47

Unapoingia katika mitandao wa kijamii, unakutana na watu wa aina mbalimbali, au makundi ya watu tofauti tofauti. Hapana ni aina kuu 10 za makundi hayo:

Wajuaji

Hawa ndio wale huamini kuwa wao ndio wanaoendesha mitaa katika mitandao ya kijamii kuanzia kuunda makundi ya WhatsApp hadi kumiliki memes. Hawa wanafahamika kwa kula bata weekend yote kuanzia Ijumaa hadi Jumapili, yani ni mwendo wa parte after parte. Wategemee kuwepo kwenye klabu/baa mbalimbali wakinywa vitu vya bei ghali, bila kusahau namna wasivyokosekana kwenye TL zao. Unaweza ukadhani hawana kazi nyingine ya kufanya.

Malkia na Wafalme

Hawa ni maarufu kwa kuwapiga watu blue tick. Yani ukiwatumia sms, hawa huisoma, hawajibu na hawajali, na mwisho wa siku hujitetea kuwa walikuwa busy, au hakuona sms yako, hata kama muda wote huo walikuwa online.

Mastaa Feki

Instagram imeleta dunia mpya kwetu, unapiga picha zako (mara nyingi nusu utupu) unapost basi hicho kinatosha kukufanya uwe model au staa. Wanaume hupata cheo cha ustaa kwa uwezo wao wa kuwalaghai wanawake, ambapo yule aliyefanikiwa kulala na wengi ndio anaonekana kidume.

Waliokua kupitiliza

Hawa huwa hawapost mara kwa mara na ni vigumu kuwaona wamepost kitu kama selfies. Huishi maisha yao kwa kujiona kana kwamba hawana haja ya kuwa active katika ulimwengu wa mitandao ya kijamii. Hata picha zao kwenye profile zao hukaa muda mrefu bila kubadilishwa, hadi kufikia watu kuwatania wakiwawata kuzibadili (si ubadili hiyo dp, kwani huchoki shingo). Unaweza ukadhani kwamba huwa hawapo online, lakini cha kwanza wao ndio wa kwanza kutazama WhatsApp Status zako, lakini huwezi kuona wakipost zao.

Wambea

Hufanya hivyo ili waonekane, wawe maarufu, wapendwe wao. Huwa wanapenda kufuatilia wenzao wanafanya nini, hasa mastaa. Watakufuatilia hasa pale unapokumbwa na skendo ambayo inachafua jina lako. Unaweza ukadhani wanalipwa kukuchafua, lakini wala. Wao hufurahia kuibua mambo mabaya katika maisha yako bila kufikiri madhara yake.

Mashine za kuchat

Ujumbe uliotumwa sekunde 10 zilizopita tayari umeshajibiwa, tena kwa jibu refu. Katika kundi hili, inakuwa ni vizuri sana ikiwa wanaohusika kuchat ni wapenzi, kuliko marafiki. Ukikutana na watu wa aina hii, lakini wewe ukawa unajibu baada ya dakika 5 au 10 huona kuwa wamedharauliwa, au hauna mood ya kuchat nao. Huweza kukaa kwenye simu zao wakichat kwa siku nzima, bila kupokea simu. Mara nyingi huwa na watu wasio na mambo ya msingi ya kufanya.

Walioumizwa

Wanawake wengi huangukia katika kundi hili. Hupenda kuposti jumbe mbalimbali zenye kuchoma hisia ambazo huwa na kundi la watu zinaowalenga, na mara nyingi jumbe hizo huwalenga wapenzi wao wa zamani baada ya kuwa wameachana. Wanawake hawa wanashauriwa kuwa makini kutokuanika hisia zao mitandaoni ambapo kila mtu atajua hali wanayopitia.

Wajasiriamali

Kundi hili huwa na lengo moja kubwa katika mitandao ya kijamii nalo ni kutengeneza fedha. Mkakati wao huwa ni rahisi, kuwavutia watu katika biashara yako, na kuwashawishi wanunue bidhaa yake. Hupunguza gharama kwa kutumia akaunti zao kuuza bidhaa na kutoa huduma kwa wateja bila kuwa na ofisi.

Akili Fyatu

Hawa hupost picha na video zenye maudhui ya ngono bila kujali ni nani atakayekuwa akiangalia, na akiwa katika mazingira gani. Hufanya hivyo kwa lengo la kupata attention ambayo huja kulingana na wanachopost. Wakati mwingine huanzisha majadiliano kwa kutumia lugha chafu, na hawaoni shida kutumia lugha ya matusi hata kama anayetukanwa hawamfahamu.

Watakatifu

Status au TL zao hujazwa na maneno ya Mungu pamoja na matangazo ya kuwaalika watu sehemu zenye mikutano ya dini au mkesha wa maombi. Unaweza ukadhani wao pekee ndio watoto pendwa wa Mungu. Kila siku ya ibada hawakosi na watahakikisha wanakujulisha kuwa wameenda kusali, na neno la siku hiyo lilikuwa ni nini. Mara nyingi hawapo vile ambavyo watu hudhani walivyo.

Send this to a friend