Aina 16 za vitabu zilizopigwa marufuku kutumika shuleni nchini

0
42

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amepiga marufuku matumizi ya vitabu 16 vinavyokwenda kinyume na maadili kwenye shule na taasisi zote za elimu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Prof. Mkenda amesema kama taifa kuna mila na desturi za kufuata na katika kufundisha na kulea watoto na kwamba shule zina wajibu wa kuendana na taratibu hizo katika kuwaandaa watoto.

“Nahimiza wazazi mkague mabegi ya wanafunzi kuhakikisha vitabu hivi havitumiki nyumbani, ukaguzi na ufuatiliaji huu ni endelevu ili kubaini kama vitabu kama hivi vipo katika shule tuweze kichukua hatua,” amesema.

Serikali kuangalia uwezekano kutoa mikopo kwa wanafunzi wa diploma na cheti

Vitabu vilivyopigwa marufuku ni pamoja na  Diary of a Wimpy Kid, Diary of a Wimpy Kid -Rodrick Rules, Diary of Wimpy Kid – The Last Straw, Diary of Wimpy Kid-Dog Days, Diary of a Wimpy Kid The Ugly Truth, Diary of a Wimpy Kid -Cabin Fever, Diary of a Wimpy Kid – The Third Wheel na Diary of a Wimpy Kid – Hard Luck.

Vingine ni Diary of a Wimpy Kid – The Long Haul, Diary of a Wimpy Kid -Old School, Diary of a Wimpy Kid -Double Down, Diary of a Wimpy Kid-The Gateway, Diary, Diary of a Wimpy Kid-Diper Overlode, Is for TANSGENDER ( you know best who you are!), Is for LGBTQIA (find the words that make you you) na Sex Education a Guide to life.

Aidha, Prof. Mkenda ametoa rai kwa Watanzania kupiga namba 0262160270 ya mezani na 0737 962965 ya mkononi ili kutoa taarifa ya uwepo wa vitabu hivyo shuleni na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa shule yoyote itakayokutwa na vitabu hivyo ikiwemo kufutiwa usajili.

Send this to a friend