Aina 5 ya mazungumzo ambayo hutakiwi kuyafanya kupitia ujumbe wa maandishi

0
20

Ingawa kutuma ujumbe wa maandishi (SMS) ni njia rahisi sana ya kuwasiliana, lakini kuna mazungumzo fulani ambayo hupaswi kamwe kuwa nayo kupitia maandishi. Maandishi yanaweza kutafsiriwa vibaya wakati mwingine na kupoteza haiba na maana yake halisi.
Haya ni mazungumzo ambayo hutakiwi kuyafanya kupitia ujumbe wa maandishi

1. Mabishano
Inaweza kuwa vigumu sana kuepuka hili lakini ni muhimu sana. Wacha tuseme wewe sio mtu wa kugombana sana, lakini kuna mtu ambaye amekukwaza. Inaweza kuwa rahisi sana kutuma ujumbe wa maandishi yanayoelezea kufadhaika kwako, badala ya kusubiri kuonana naye.
Ujumbe huo unaweza kutafsiriwa tofauti na kile ulichokikusudia, hivyo ni vyema kuonana au kuzungumza naye kwa njia ya simu kusikia sauti ya mtu huyo na kupata majibu kwa haraka.

2. Kuvunja mahusiano
Kamwe usiwahi kuachana na mwenzi wako kupitia ujumbe wa maandishi. Kwanza kabisa, unapaswa kumheshimu mtu uliye naye vya kutosha na kumuonesha heshima ya kuachana naye kwa njia ifaayo, lakini si kwa maneno machache ya ujumbe wa maandishi.
Kuachana si rahisi, hivyo itawafanya wahisi kuumia zaidi, kuchanganyikiwa, kuhisi kukataliwa na pia haimpi mtu yeyote nafasi ya kusema mambo anayohitaji kusema.

Aina 6 za smartphones bora zaidi unazoweza kununua

3. Kuelezea hisia zako
Inashauriwa kuwa unapotaka kueleza hisia zako kwa mtu unayemuhitaji, basi jitahidi uongee naye ana kwa ana badala ya kumtumia ujumbe mfupi.
Majadiliano ya ana kwa ana huruhusu muunganiko na ushirikiano wa kweli na kutoa nafasi zaidi kwa kila mtu kusikilizwa na kuzingatiwa.

4. Mazungumzo muhimu ya kibiashara
Ikiwa una jambo muhimu la kibiashara kama vile kuomba kazi, kuacha kazi au mazungumzo yoyote muhimu ya kibiashara basi usitume ujumbe wa maandishi isipokuwa kuonana naye ana kwa ana.

5. Habari za kushtua
Ikiwa kuna ujumbe utakaomshtua mtu kama vile taarifa za kifo au ugonjwa mbaya, haishauriwi kumtumia mtu ujumbe wa maandishi kwakuwa hufahamu mtu huyo yupo katika hali gani kwa wakati huo. Hii inaweza kufanya mambo yawe mabaya zaidi, badala yake ni bora kufanya mazungumzo naye kwa njia ya simu na kusikia sauti yake.

Send this to a friend