Aina 5 za magari yanayotumia mafuta mengi zaidi

0
40

Ikiwa wewe ni mpenzi wa magari au umepanga kununua gari hivi karibuni ni vyema kutambua aina ipi ya gari ambayo unaweza kuimudu katika nyanja zote ikiwemo utumiaji wake wa mafuta.

Kuna aina tofauti za magari, katika aina hizo hutofautiana katika upande wa matumizi ya mafuta, yapo yanayotumia mafuta kidogo, na mengine yanayotumia mafuta mengi ambayo haya kiuhalisia huwa na gharama kubwa hata kwenye upande wa manunuzi na matengenezo yake pia.

Fuatilia orodha hii ya magari ambayo yanatumia mafuta mengi zaidi;

Toyota Landcruiser V8
Haya ni magari mazuri sana, yanayopendwa sana nchini hasa na viongozi wa Serikali na watu wenye pesa. Kabla hujapanga kununua gari hili ni vyema ukafahamu kuwa lina ulaji mkubwa wa mafuta lakini ni gari zuri sana kwa matumizi ya kusafiria masafa marefu.

Marcedez Benz Brabus 800
Inaelezwa kuwa gari hili hutumia zaidi ya lita 13 za mafuta ukitembea kilometa 100. Magari haya ni ya kifahari na yanauzwa kwa bei ghali.

Aina za magari bora zaidi kwa wanawake kuyatumia

Jeep Wrangler
Jeep Wrangler ni magari yanayosifika sana katika matumizi ya shughuli za kijeshi na safari katika barabara za mazingira magumu. Magari haya hutumia mafuta mengi sana na huuzwa kwa gharama kubwa. Inaelezwa kuwa lita moja ya mafuta inatembea kilomita 9 pekee.

Hummer H2
Gari hili pia linasifika kutumia mafuta kwa wingi ambapo inadaiwa kuwa kwa lita 1 ya mafuta hutembea kilometa 5 tu, hivyo ni vyema kuwa na uhakika wa kumudu mafuta vinginevyo unaweza kulipaki tu nyumbani.

Rolls Royce
Gari hili linahitaji mafuta mengi kwa ajili tu ya kutembea mwendo mdogo, hii ni kwa sababu yana injini kubwa, nzito, zenye nguvu zaidi kuliko za kawaida ambazo zinahitaji mafuta zaidi ili kuongeza kasi. Pia lina uwiano wa chini wa gea ambao hufanya gari kuhitaji mafuta zaidi ya kutumia.