Kujaribu kitu kipya kunaweza kuwa na faida lakini pia kunaweza kuwa na madhara. Wataalamu wanashauri watu kula vyakula wanavyovijua kwani vitakuwa na faida na havitawasababishia matatizo yoyote.
Kwa mujibu wa wataalam wa afya, kuna aina nyingi ya vyakula ambavyo vikichangwanywa vinaweza sababisha madhara kwenye mwili wa binadamu na hata kusababisha kifo.
Hivi ni baadhi ya vyakula hivyo;
Samaki na Maziwa
Mwili wa binadamu hauhitaji vyakula vya aina tofauti vyenye kemikali za aina moja kuchanganywa, kwani vinaweza kusababisha sumu itakayopelekea mtu kutapika na hata kuharisha. Samaki na Maziwa ni vyakula vyenye virutubisho vingi na kuvichanganya katika sehemu moja vinaweza visiwe na uwezo wa kutengeneza virutubisho sahihi.
Haya ndiyo madhara ya kuchelewa kula chakula usiku
Maji ya limao na Maziwa
Maji ya limao na maziwa haviwezi kukaa sehemu moja, kwani vikichanganywa lazima maziwa yakatike. Ikiwa mtu atachanganya maziwa na maji ya limao anaweza kutengeneza sumu, vilevile yanaweza kumletea shida kwenye moyo.
Mafuta ya mzeituni na Karanga
Karanga ni muhimu sana katika mwili wa binadamu na hutumika katika sehemu nyingi. Karanga ina kiwango kikubwa cha protini na wanga, pia ni moja ya virutubisho muhimu katika lishe.
Mafuta ya mzeituni husaidia hasa katika masuala ya tiba kwa baadhi ya magonjwa. Mchanganyiko wa mafuta ya mzeituni na karanga unaweza kuleta shida, ndio maana inashauriwa kutumika pale kimoja kinapokosekana lakini sio vyote kwa pamoja.
Dawa pamoja na limao/soda zenye gesi
Limao au kinywanji chochote chenye gesi hakipaswi kuchanganywa na dawa, ni hatari. Kuchukua dawa na kuchanganya na kitu chenye gesi ina madhara makubwa, wataalamu wanasema kunywa dawa na soda kama fanta au Coca-Cola inaweza kukusababishia kifo kutokana tu ongezeko kubwa la gesi.
Nyama na mayai mabichi
Kuchanganya nyama ambayo haijaungwa na mayai mabichi inaweza kusababishia matatizo katika mwili wa binadamu. Inaweza kuwa sumu na zingine zinaweza kusababisha kutapika na kuhara kwa sababu haifai kutumika hivyo.
Nyama mbichi inaweza kusababisha athari ikiwa usindikaji wake haufuatwi ili kupunguza kiwango cha virutubishi vilivyomo.
Chanzo: BBC Swahili