Aina 6 za vyakula vinavyosababisha Saratani unavyokula kila siku

0
61

Mwanadamu anahitaji chakula ili kuupa mwili nguvu aweze kuishi na kutekeleza majukumu yake ya kila siku. Lakini katika mchakato huo, wakati mwingine anakula vyakula ambavyo vinamuweka katika hatari mbalimbali, kubwa ikiwa ni kupata magonjwa au kufariki.

Zifahamu aina sita za vyakula ambazo hutumiwa kila siku na watu mbalimbali ambavyo vinaweza kusababisha saratani:

1. Vyakula vya vilivyobadilishwa vinasaba (genetically modified organism)
Vyakula hivi huwa na kemikali mbalimbali kama herbicides na sumu za wadudu kama vile atrazine pamoja na kemikali zitokanazo na mbolea. Vitu vyote hivi vinaweza kusababisha madhara kwenye viungo vya mwili wako hasa vinapotumiwa kwa wingi.

2. Chips
Si tu zinaongeza uzito, bali pia zinahusishwa na kusababisha saratani kutokana na kuwa na sodium nyingi ambayo kwa watu wengi husababisha shinikizo la juu la damu. Pia chakula hicho kina wingi wa mafuta yanayoongeza cholestrol mwilini.

3. Unga wa ngano uliochakatwa zaidi
Viwanda vingi vimekuwa na utaratibu wa kung’arisha unga kwa kutumia gesi ya chlorine, tofauti na miaka ya nyuma ambao unga huo uliachwa ukang’aa wenyewe baada ya muda. Gesi hiyo si salama kuiingiza ndani ya mwili, na ikiwa kwa kiwango kikubwa inakuwa hatarishi.

4. Sukari iliyosafishwa (refined)
Kuenea kwa saratani mwilini huwa kwa kasi kubwa endapo mwathirika atatumia vitu vya sukari. Ukiwa katika hatari hiyo, inashauriwa kuepuka vyakula vyenye sukari ili kujiweka salama.

5. Vilevi
Vinashika nafasi ya pili kwa kusababisha saratani. Wakati unywaji wa wastani unaweza kuwa na faida katika mwili na kupunguza madhara ya maradhi ya moyo, unywaji uliopindukia unasababisha moyo kushindwa kufanya kazi, kiharusi, vifo vya ghafla, pia, huathiri figo na ini.

6. Nyanya ya kopo
Vyakula vingi vya kusindikwa si salama kwa afya yako kwa sababu hutengenezwa kuwa kutumia kemikali aina ya bisphenol-A, au BPA. Nyanya ni hatari zaidi kutokana na kiwango kikubwa cha acid ambayo hukwangua kopo la bati, na hivyo kupelekea vipande vipande vya kopo hilo kuingia kwenye nyanya.