Aina 7 za magari imara yanayotengenezwa Afrika

0
103

Karibu magari yote yanayopatikana barani Afrika huagizwa kutoka nje na hivyo kuchangia kuwa ghali kutokana na uwepo wa kodi ya kuyaingiza katika nchi husika.

Hata hivyo viwanda vya utengenezaji magari Afrika havijabaki nyuma katika mapambano ya kuleta mapinduzi kufanikisha gharama ndogo za bidhaa hiyo.

Hapa chini ni viwanda saba vya magari Afrika ambavyo vinabadili hadithi ya upatikanaji wa magari Afrika.

1. Birkin Cars (Afrika Kusini)

Is it really worth it buying made in Africa cars? The pros and cons, as  well as examples | naijauto.com
Kampuni hii ilianza mwaka 1982 na huenda ikawa ndio kampuni kongwe zaidi ya magari Afrika. Magari yanayozalishwa na kiwanda hicho huuzwa katika nchi mbalimbali duniani ikiwamo Marekani, Japa na barani Ulaya.

2. Innoson Motors (Nigeria)

Innoson Motors and Evolution of Global Post-War Vehicle Manufacturers -  Tekedia
Ilianzishwa na mjasirimali wa Nigeria, Innocent Chukwuma, ambapo imezalisha takribani magari 500 ambapo baadhi hutumiwa na maafisa wa serikali.

Kampuni hii pia huunganisha magari mbalimbali ambayo baadhi ni pamoja na pickup, SUVs na mabasi. Baadhi ya modeli za kampuni hii ni Innoson Fox, Innoson Umu, na Innoson G5.

3. Kantanka Cars (Ghana)

Ghana's locally produced 'Kantanka' cars grab market share | Daily Sabah
Kampuni hii imeanzishwa nchini humo na Dr Ing. Kwadwo Safo Kantanka. Huzalisha magari madogo na makubwa (SUVs) ambazo ni pamoja na Nkunimdie na Kantanka Opasuo.

Kampuni hii ilitangaza kuanza kuzalisha magari ya umeme mwishoni mwa mwaka 2020.

4. Kiira Motors Corporation (Uganda)

Building African Cars, the Kiira Way - Ventures Africa
Utofauti wa kampuni hii na nyingine za Afrika ni kuwa inatengeneza magari yenye mifumo miwili ya nishati endeshi (hybrid electronic vehicle). Ilianzishwa mwaka 2014 na mwanafunzi wa uhandisi wa Chuo Kikuu cha Makerere aliyeshiriki mkutano wa ubunifu magari ulioandaliwa cha Chuo ha Teknolojia Massachusetts (MIT) mwaka 2006.

Inazalisha aina za magari kama Kayyoola Solar Bus, Kiira EV Smack, na Kiira EV POC.

5. Laraki (Morocco)

Laraki Automobiles SA - Nyongesa Sande
Mfanyabiashara wa Morocco, Mohamed Laraki alianzisha kampuni hii mwaka 1999 ambapo ilianza kwa kutengeneza boti (Yatch), na baadaye ikahama na kuanza kutengeneza magari ya kifahari. Mwaka 2002 ilizalisha gari lake la kwanza linaloitwa Laraki Fulgura.

Magari yake yalitajwa katika orodha ya magari ghali zaidi duniani mwaka 2015, yakiuzwa kwa gharama ya zaidi ya TZS bilioni 4.6.

6. Mobius Motors (Kenya)

The luxury SUV made in Kenya, for Africans | CNN
Kampuni hii ilianzishwa mwaka 2010 kwa ajili ya soko la Afrika, na awamu ya kwanza ya magari yake ya bei nafuu yalitolewa kuelekea mwishoni mwa 2020.

Kampuni hiyo inatumia ubinifu uliorahishwa kuzalisha magari imara kwa bei nafuu ili kushindani na magari ya mtumba ambayo yametawala soko la Afrika Mashariki. Magari hayo hugharimu takribani milioni 23.

7. Wallyscar (Tunisia)

WALLYSCAR - IRIS
Ilianzishwa mwaka 2006, na kampuni hiyo inafahamika kwa kuunda magari nafuu, tegemeo na imara 4×4.

Ripoti ya mwaka 2014 inaonesha kuwa kampuni hiyo huu za magari 600 kwa mwaka, mengi yakiuzwa Afrola na Mashariki ya Kati.

Send this to a friend