Aina sita za mavazi unayoshauriwa kutokuvaa kwenye harusi

0
73

Kuchagua mavazi yako ya harusi inapaswa kuwa makini pia. Unachohitajika kufanya ni kujiweka katika viatu vya bibi harusi na kufikiria juu ya kile angetaka kuona katika siku yake kuu.

Hivi ni vitu sita ambavyo hutakiwi kuvaa unapohudhuria sherehe ya harusi.

Nguo nyeupe
Kuvaa nguo nyeupe kwenye harusi si jadi nzuri, isipokuwa wewe ni bibi harusi au maharusi wametaka wageni wavae nguo nyeupe. Bibi harusi anastahili kusimama katika vazi lake, na hutakiwi kumfadhaisha au kuwafadhaisha wageni wengine kwa kuvaa chochote anachotakiwa kuvaa bibi harusi.

Jeans na sneakers.
Haijalishi ikiwa sherehe ni ya kawaida, jeans, T-Shirts na sneakers hazifai kamwe kuvaa kama mgeni wa harusi. Onesha heshima kwa bibi na bwana harusi kwa kuvaa rasmi. Ni vema ukavalia koti na tai au shati la mikono mirefu na suruali ya kitambaa. Hiyo itaonyesha kuheshimu sherehe hiyo.

Mwonekano uliopitiliza.
Moja ya sheria kubwa za kuvaa kwa ajili ya harusi ni kamwe kutowashinda bibi na bwana harusi. Epuka mapambo yanayometa sana,  visigino virefu sana au mavazi mengine ambayo yatavuta umakini kutoka kwa bibi harusi. Kumbuka harusi sio wakati unaofaa wa kuonesha umahiri wako wa mitindo.

Kaptura
Hata ikiwa una miguu mizuri ya kuvutia kiasi gani, kaptula sio chaguo zuri kwenye harusi. Hata katika majira ya joto, hata katika harusi ya kawaida zaidi, kifupi sio nzuri kwa siku kama hiyo. Kuna mitindo nadhifu na mizuri zaidi ya kuvaa kwenye harusi hivyo huna sababu ya kuvaa kaptula.

Mtupu
Ikiwa umepanga kuvaa nguo itakayoacha sehemu kubwa ya mwili wako wazi, hicho sio kitu ambacho bibi harusi wengi wangependa kuona katika siku yao. Vaa vizuri na ujizuie kuonyesha mwili wako. Harusi ni kuhusu bibi harusi, si kuhusu wageni.

Nguo zenye chapa na Tshirt

Haijalishi ikiwa t-shirt yako ni nzuri namna gani, sio mahali pa kuivaa. Ikiwa unapanga kuvaa koti nzuri juu yake huenda ikawa sawa. Epuka kuvaa nguo yenye chapa kubwa kifuani kwenye sherehe ya harusi badala yake tafuta chaguo litakaloendana na aina hiyo ya sherehe.

 

Send this to a friend