Utafiti uliofanywa na mwalimu wa saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Dalhousie unaonesha kuwa, watu ambao wanasubiri muda sahihi ili kutimiza jambo fulani pasipo kuchukua hatua ya kuanza kutekeleza malengo yao, huwa wanachelewa kufanikiwa.
Na hizi ni sababu zifuatazo;
• Huwa wanatumia muda mwingi sana kukamilisha lengo moja.
Watu wanaopenda ukamilifu wa kila kitu kabla ya kuchukua hatua, huwa wana tabia ya kusubiri yawe kama vile wanavyotaka. Ukiuliza kwanini hujaanza biashara, watajibu bado mazingira hayajakamilika. Watu wa namna hii, wana mawazo lakini hawana vitendo.
• Huwa ni watu wa kuhairisha mambo
Jambo linalohitajika kufanyika sasa, wao husema ‘nitafanya kesho’ huwa na mipango mingi ambayo huisimulia kwa watu, lakini nusu ya mwaka unaweza kupita bila kutimiza hata lengo moja na badala yake husogeza mipango yake mbele.
• Huwa wanakatishwa tamaa na mambo madogo madogo
Watu wa namna hii hukatishwa tamaa na mambo madogo yanaposhindwa kufanikiwa au watu wanaowazunguka na hivyo kusahau ndoto kubwa ya maisha yao waliyonayo mbeleni.