Aina za mali zisizoweza kugawanywa pindi wanandoa wanapotengana

0
24

Kufuatia mijadala mingi ndani ya jamii juu ya aina ipi za mali ambazo zinafaa kugawanywa kwa wanandoa pindi wanapoamua kutengana, Hakimu Mkazi Mwandamizi Kituo Jumuishi Temeke, Elias Migella amesema zawaidi zinazotolewa wakati wa sherehe kabla ya ndoa kama vile ‘send off’ na ‘kitchen party’ haziwezi kugawanywa kwani ni mali binafsi.

Akizungumza katika kipindi cha Sema na Mahakama, Hakimu Migella amesema endapo familia itatamka mbele ya umati kwamba zawadi hizo ni za wanandoa ushahidi huo utatumika mahakamani kuthibitisha kwamba mali hizo ni za pamoja.

Fanya mambo haya matano kusahau kumbukumbu mbaya akilini mwako

Amefafanua kuwa wapenzi au wachumba wanaonunuliana zawadi kama vile magari, nyumba au kulipa ada za masomo kabla ya ndoa wanapoachana watu hao wanaweza kufungua kesi ya madai kudai kulipwa fidia, na kwamba mali iliyotolewa na mke au mume kwa mwenzi wake ni mali binafsi kwa aliyepewa hivyo haipaswi kujumuishwa kama mali za pamoja.

Ameongeza kuwa kifungu cha 160 (1) cha sheria ya ndoa iliyofanyiwa marejeo mwaka 2019, kinatambua mahusiano kuanzia miaka miwili, katika mgawanyo wa mali wenza hao watahitaji kuwa na ushahidi kwamba waliishi kama mke na mume na jamii inawachukulia hivyo.