Aiomba Serikali imwajiri anyonge wafungwa

0
22

Mmoja wa washiriki wa mkutano wa haki jinai Kibaha mkoani Pwani, Ramadhan Maulid ameeleza kuwa anatamani serikali ingemuajiri ali afanye kazi ya kunyonga watu waliohukumiwa adhabu hiyo na mahakama.

Ameeleza kuwa maamuzi hayo ni kutokana na kile kinachoelezwa kuwa adhabu hiyo haitekelezwi kwa zaidi ya miaka 10 huku matukio mbalimbali ya mauaji yakiendelea nchini.

“Haiwezekani mtu anaua kwa makusudi halafu anaenda kukaa gerezani miaka na miaka bila kunyongwa hilo haliwezekani, kama mtu amekutwa na hatia ya kunyongwa na yeye anyongwe, lakini sio unasikia wengine wanaanza kusema haki za binadamu, kwani yeye alipokuwa anaua alikuwa hajui kuwa kuna haki za binadamu?” amehoji huku akitaka serikali iajiri watu wenye roho ngumu kama yeye aweze kufanya kazi hiyo

Akamatwa kwa kumuua mumewe kwa rungu akiwa amelala

Aidha, Mjumbe wa Tume hiyo, Profesa Edward Hosea amesema katika ufuatiliaji wao wamebaini kuwa sheria nyingi zinatakiwa kufanyiwa marekebisho ili kulinda haki za wananchi.

Send this to a friend