Ajali yaua 18 Mafinga

0
38

Watu 18 wamefariki dunia kufuatia ajali ya gari iliyohusisha basi dogo aina ya Costa na lori la mizigo eneo la Changarawe, Mafinga mkoani Iringa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

“Ni kweli ajali imetokea na inasadikika watu zaidi 10 wamepoteza maisha papo hapo,” amesema Kamanda Bukumbi.

Aidha, baadhi ya mashuhuda walio katika eneo la tukio wamesema jitihada za kuokoa majeruhi na kutoa miili ya watu zinaendelea.

Send this to a friend