Ajifanya askari polisi na kulawiti watoto 15 Iringa

0
43

Jeshi la Polisi mkoani Iringa linamshikilia dereva wa bajaji anayetambulika kwa jina la Alex Msigwa, kwa tuhuma za kuwabaka na kuwalawiti watoto 15 katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Iringa.

Akizungumza na vyombo vya Habari, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Allan Bukumbi amesema mtuhumiwa huyo aliyekuwa akijifanya afisa ustawi wa jamii na wakati mwingine Askari Polisi alikuwa akiwakamata watoto wanaozurura na kutembea usiku kisha kuwafanyia ukatili huo.

Ameongeza kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa akiwatishia kwa kisu watoto hao wenye umri kati ya miaka sita hadi 12 na wakati mwingine akiwapatia fedha.

Aidha, Kamanda Bukumbi amewasihi wazazi kuwa karibu na watoto wao na kuacha kuwatuma dukani hasa nyakati za usiku.

Send this to a friend