Ajifanya daktari na kuwafanyia wagonjwa upasuaji wa mabusha

0
25

Jeshi la Polisi wilayani Ludewa mkoani Njombe linamshikilia Abdallah Athumani (43), mkazi wa Kijiji cha Mapogolo kwa tuhuma za kutoa matibabu kwa wagonjwa hospitalini pasipokuwa na vyeti vya kitaaluma.

Ameeleza hayo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Mahamoud Banga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo ambapo amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa akiwa na boksi zaidi ya 23 za vifaa tiba vinavyotumika hospitalini, na amekuwa akiwatibu watu mbalimbali kwa kufanya upasuaji mdogo kama kuondoa mabusha na tezi dume.

Dawa za uchungu za mitishamba zinavyoongesha vifo vya wajawazito

Aidha, Kamanda Banga amesema katika tukio hilo hilo, jeshi hilo limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mwingine aliyetambulika kwa jina la Ibrahim Mgimba (25) kwa kushiriki kusafirisha vifaa tiba hivyo na kuvificha.

Jeshi limesema watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Send this to a friend