Ajifungua mahakamani baada ya kuachiwa kwa tuhuma za mauaji

0
47

Virginia Maingi amejifungua katika mahakama ya Kithimani, Kaunti ya Machakos nchini Kenya baada ya mahakama hiyo kumwachia huru kwa tuhuma za mauaji.

Mwanamke huyo alikamatwa Machi 25 mwaka huu baada ya kifo kilichotiliwa shaka cha mtoto wake aliyekuwa na umri wa mwaka mmoja na miezi saba na kuzuiliwa kwa ajili ya uchunguzi ambapo alifikishwa mahakamani Machi 27.

Baada ya kupandishwa mahakamani Aprili 15, mahakama ilimwachia huru baada ya uchunguzi wa kitabibu kubaini kuwa mtoto wake alifariki kwa njaa.

Muda mfupi baada ya kuachiliwa, Virginia alipata uchungu wa uzazi katika majengo ya mahakama, na kuwafanya makarani wa mahakama kuwaita mara moja wauguzi kutoka zahanati iliyo karibu na kumhudumia mara moja.

Send this to a friend