Ajikuta ndani ya jeneza amezikwa futi sita baada ya kulewa kupita kiasi

0
39

Mwanaume mmoja anayejulikana kwa jina la Victor Hugo Mica Alvarez (30) , mkazi wa Amerika Kusini ya Bolivia, amejitokeza na kueleza jinsi alivyoishia kuzikwa akiwa hai ndani ya jeneza baada ya kulewa kupita kiasi.

Mwanaume huyo alishtuka na kujikuta yuko ndani ya jeneza katika shimo lenye urefu wa futi sita chini ya ardhi baada ya kuzimia katika jiji la El Alto nchini Bolivia.

Inadaiwa, Alvarez alikunywa pombe nyingi usiku uliopita katika ufunguzi wa tamasha la Pachamama (tamasha la Mama Duniani), ambapo watu hutoa shukrani kwa miungu.

Mume kizimbani kwa kutishia kumuua mke kisa kupeleka chakula kwa mchungaji

Alvarez anaamini kwamba wafuasi waliokuwa katika tamasha hilo, walimzika akiwa hai kama sadaka yao kwa mungu wa kike ambapo huamini kwamba, mungu wa kike hufungua kinywa chake kwa ajili ya kupokea matoleo yao kila ifikapo Agosti.

“Jana usiku ilikuwa ni kipindi cha kabla ya tamasha, tulikwenda kucheza. Na baadaye, sikumbuki. Kitu pekee ninachokumbuka ni kwamba nilifikiri nilikuwa kitandani kwangu, nilitaka kuinuka kwenda haja ndogo na sikuweza kusogea.”amesimulia.

Ameeleza, “Niliposukuma jeneza niliweza kuvunja glasi iliyokuwepo nayo na kwa njia hiyo niliweza kutoka. Walitaka kunitumia kama sadaka.”

Ameendelea kueleza jinsi alivyofanikiwa kujinasua kutoka kwenye shimo dhidi ya tope lililokuwa limerundikana “Nilivunja kioo, mkono wangu wote ulikuwa umeumia, nilitoka kwa shida, lakini nilienda polisi wakaniambia nimelewa.

Alvarez aliporipoti tukio hilo katika kituo cha polisi, lakini walikataa kumwamini na kumwambia kwamba alikuwa amelewa sana, hivyo zilikuwa ni akili ya pombe tu.

Send this to a friend