Ajinyonga akimtuhumu mke wake kumsaliti na kijana wa mtaani

0
55

Amani Ibrahim mwenye umri wa miaka 27 mkazi wa Ibungiro C Jijini Mwanza amejiua kwa kujinyonga kwa madai ya kumtuhumu mke wake kuwa anamsaliti na mwanaume mwingine.

Mama mzazi wa kijana huyo, Sarah Ibrahim amesema huenda changamoto za kimahusiano alizokuwa nazo kati yake na mke wake ndizo zimepelekea kuchukua maamuzi hayo ya kujiua.

Akizungumza Kamanda wa Polisi mkoani humo, Wilbrod Mutafungwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema baada ya uchunguzi kufanyika wamekutana na ujumbe ambao unadhaniwa kuandikwa na marehemu akimtuhumu mkewe kumsaliti na kijana wa mtaani.

“Kuna karatasi ambayo imekutwa chumbani ambayo tunadhani imeandikwa na yeye mwenyewe marehemu karatasi hiyo ina maneno inayosema yeye ameamua kujiua kwasababu ya mapenzi kwamba anamtuhumu mke wake kuwa na mahusiano na kijana mmoja hapo mtaani, na akaeleza kwamba kifo chake kisihusishwe na mtu yeyote,” ameeleza.

Send this to a friend