Ajira milioni 14 kutoweka ndani ya miaka 5 ijayo

0
44

Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) limesema kufikia mwaka 2027 nafasi mpya za kazi milioni 69 zitaundwa, na kuondolewa kwa nafasi milioni 83 ambapo itasababisha hasara ya jumla ya ajira milioni 14, sawa na asilimia 2 ya ajira za sasa.

Ripoti ya WEF inaeleza sababu mbalimbali zitakazopelekea mtikisiko wa soko la ajira katika kipindi hicho ikiwemo mabadiliko ya mifumo ya nishati mbadala ambayo itazalisha ajira kwa wingi, huku ukuaji taratibu wa uchumi na mfumuko wa bei ukisababisha hasara.

Kampuni zitahitaji wafanyakazi wapya ili kusaidia utekelezaji na udhibiti wa akili bandia (artificial intelligence) huku ajira za wachanganuzi wa data na wanasayansi, wataalamu wa kujifunza kwa mashine na wataalam wa usalama wa mtandao zinatabiriwa kukua kwa wastani wa asilimia 30 ifikapo mwaka 2027, kulingana na WEF.

Kwanini watu huweka ‘airplane mode wakiwa ndani ya ndege?

Mashirika yaliyohojiwa na WEF yamekadiria kuwa, asilimia 34 ya kazi zote zinazohusiana na biashara kwa sasa zinafanywa na mashine huku makarani wa uandikishaji data na makatibu wakuu wanatarajiwa kuathirika zaidi.

Mnamo 2020, waajiri walidhani asilimia 47 ya majukumu yangekuwa ya kiotomatiki kufikia 2025, sasa wanatarajia idadi hiyo kuongezeka hadi asilimia 42 kufikia 2027.