Ajirusha mtoni baada ya kudhihakiwa baa kwamba hawezi kupigana

0
47

Timu ya kudhibiti majanga nchini Kenya inaendelea na msako wa kumtafuta mwanaume anayedaiwa kuruka kwenye mto uliokuwa umejaa maji baada ya kudhihakiwa na marafiki zake baa wakiwa wanakunywa pombe.

Inaelezwa kwamba marafiki zake marehemu walikuwa wakimcheka kutokana na uwezo wake mdogo wa kupigana, hali iliyomfanya ajisikie vibaya na kufikia hatua ya kujaribu kujiua.

Mwanaume huyo alionekana kukabiliwa na msongo wa mawazo baada ya mmoja wao katika kundi hilo kutishia kutumia makofi ili kumweka chini na kuamua ni nani anapaswa kuongezwa pombe zaidi.

Juhudi za marafiki zake kumtuliza hazikuzaa matunda, kwani aliendelea kuwa na msimamo wake wa kutaka kuondoka eneo hilo na hatimaye alionekana kuelekea mtoni umbali wa kilomita moja kutoka hapo.

Hata hivyo kulingana na mjomba wa marehemu, Paul Sang baadhi ya nguo vinavyodhaniwa kuwa vya marehemu vilipatikana karibu na Mto Chepkulo, ambapo inaaminika alionekana akielekea baada ya mzozo huo.

Chifu wa eneo hilo, Joseah Ng’eno amesema uchunguzi unaendelea kubaini sababu kamili za tukio hilo.

Send this to a friend