Ajiua baada ya kukuta sms za mchepuko kwenye simu ya mumewe

0
59

Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limethibitisha kifo cha mwanamke anayefahamika kwa jina la Marietha Bosco (32) mkazi wa kijiji cha Marungu wilaya ya Nyasa ambaye amejiua kwa dawa ya kuulia wadudu baada ya kukuta jumbe za mwanamke mwingine kwenye simu ya mumewe.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Marco Chilya ameeleza kuwa Novemba 08, mwaka huu baada ya mume wa marehemu kwenda shambani, mwanamke huyo alichukua simu ya mume wake na kuanza kupekua jumbe mbalimbali kwenye simu hiyo, na ndipo alipokuta jumbe za mwanamke mwingine ambaye ni mchepuko wa mume wake.

“Katika kuangalia zile messages akakuta jumbe nyingi za chatting kati ya mume wake na mwanamke mwingine, ndipo marehemu akashindwa kuvumilia jumbe zilizokuwepo katika ile simu na hivyo akachukua dawa ya kuulia wadudu ya mahindi inaitwa actellic akaichanganya na kuinywa. Baada ya kuja majirani aliwaambia kuwa amekunywa dawa ya kuulia wadudu baada ya kukuta message kwenye simu ya mume wake,” ameeleza.

Send this to a friend