Ajiua kwa kunywa sumu akihofia kudaiwa TZS 47,000 za soda 

0
61

Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la Bukindu Mhoja (22) Mkazi wa Kijiji cha Bukoli, Kata ya Bukoli mkoani Geita amefariki dunia baada ya kunywa sumu akihofia kudaiwa elfu 47,000.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi Ally Kitumbu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kijana huyo amefariki kwa kunywa sumu na kwamna jeshi hilo likiendelea na uchunguzi zaidi wa tukio hilo.

Mama wa marehemu amesema kijana huyo aliagizwa dukani kununua soda alipofika dukani akatoa pesa ili ahaudumiwe lakini  alipotaka kubeba soda hizo  mwenye duka  alimwambia bado hajalipa hali iliyosababisha kijana huyo kurudi nyumbani na kuchukua uamuzi wa kunywa sumu.

Send this to a friend